TFF YATUPILIA MBALI RUFAA YA POLISI DAR
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), limepokea rufaa kutoka Klabu ya Polisi Dar es Salaam dhidi ya
Klabu ya Simba kuhusu kumchezesha Mchezaji Novalty Lufunga katika mchezo wao wa
Raundi ya Tano ya Kombe la Azam Sports Federation Cup 2017.
Madai ya Polisi ni kwamba
Mchezaji Novalty Lufunga alioneshwa kadi nyekundu kwenye Simba dhidi ya Coastal
Union katika mchezo wa Azam Sports Federation Cup 2015/2016 uliofanyika Uwanja
wa Uhuru, Januari 22, mwaka huu.
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) limetupilia mbali rufaa hiyo kwa kukosa vigezo vya kikanuni
katika uwasilishaji wake na hivyo kukosa sifa ya kusikilizwa. Hii ni kwa mujibu
wa kanuni ya 18 (1) na (2) ya Kanuni za Kombe la Shirikisho la Azam Sports HD.
Kanuni ya 18 (1) inasema: “Malalamiko
yoyote kuhusiana na mchezo yawasilishwe kwa maandishi kwa kamishna wa mchezo au
TFF sio zaidi ya masaa sabini na mbili (72hrs) baada ya kumalizika mchezo.”
Kanuni ya 18 (2) inasema: Ada ya
malalamiko ni shilingi laki tatu (Tshs 300,000.00). Malalamiko yo yote
yatakayowasilishwa bila kulipiwa ada na kuwasilishwa nje ya muda uliowekwa
hayatasikilizwa.”
Hata hivyo, Shirikisho linapenda
kutoa ufafanuzi kuhusu kadi nyekundu aliyopewa Mchezaji Novalty Lufunga katika
mashindano ya Azam Sports Federation Cup 2016/2017.
Kwa utaratibu wa mashindano haya
ambayo ni ya mtoano, adhabu za kadi (njano na nyekundu) zitolewazo uwanjani,
zinakoma mwisho wa msimu wa shindano husika isipokuwa kadi hizo zikiongezwa
adhabu ya kinidhamu (suspension) ambayo itafahamisha kwa klabu na mchezaji kwa
maandishi.
Kadhalika, Kanuni ya 16 ya Kanuni
za Kombe la Shirikisho Sehemu ya Tatu inaeleza wazi kuwa matumizi ya kanuni za
ligi zitahusika maeneo yanayoruhusu uendeshaji wa shindano la mtoano.
“Adhabu zote zinazohusisha katika
mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam HD zitahusisha na shindano hili tu,”
inasema kanuni ya 16 (3) na (4).
No comments