EFL: PAUL POGBA AIPELEKA MAN UNITED FAINALI
Goli pekee la ugenini lililofungwa na mchezaji ghali kwa sasa duniani Paul Pogba lilitosha kuwapa Man United Tiketi ya kucheza fainali ya michuano ya kombe la ligi nchini England (EFL)
Pogba alifunga bao hilo katika mechi ambayo Man United ilikubali kichapo cha bao 2-1 toka kwa Hull City katika mechi ya pili ya nusu fainali baina ya timu hizo kwenye dimba la Kingston Communication jijini Hull.
Wakionyesha soka safi Hull City walifanikiwa kupata bao la kuongoza kipindi cha kwanza kwa njia ya penati baada ya Marcos Rojo kumwangusha mmoja wa wachezaji wa Hull wakati wakigombania mpira wa kona kwenye lango la United na kiungo Tom Huddlestone akifunga bao hilo.
Kipindi cha pili Paul Pogba aliweza kuisawazishia Man United akifunga goli kwa mpira uliopigwa na Huddlestone ambaye alikua katika harakati za kuokoa mpira ambao ndilo haswa lililokua likihitajika ili United wavuke kwenda fainali kufatia matokeo ya mechi ya awali ambayo United iliweza kuibuka na ushindi wa bao 2-0.
Bao la pili la Hull City ambao walionekana kuelewana vilivyo lilifungwa na kiungo mshambuliaji Baye Oumar Niasse baada ya mabeki wa United kushindwa kumzuia mfungaji.
Kwa matokeo hayo Manchester United itacheza dhidi ya Southampton katika fainali itakayochezwa katika uwanja wa Wembley.

No comments