SIMBA YALIZWA TENA NA AZAM SASA MBIO ZA UBINGWA NI HESABU ZA MAGAZIJUTO

Mbio za ubingwa kwa Vinara wa ligi kuu Tanzania bara Simba sawa zinategemea hesabu zaidi ya pointi ilizonazo baada ya leo kukubali kufungwa bao 1-0 na Azam FC.
Huu ni mchezo wa pili mfululizo Simba inapoteza bao 1-0 dhidi ya Azam FC baada ya kupoteza katika mchezo wa fainali ya kombe la Mapinduzi mjini Zanzibar.

Mchezo wa leo ulitawaliwa zaidi na Simba ambao walikosa nafasi nyingi huku Azam wakicheza kwa uangalifu mkubwa na kufanikiwa kupata bao pekee lililofungwa na nahodha John Bocco dakika ya 70 ya Mchezo kufatia makosa ya beki wa Simba Method Mwanjale aliyeshindwa kuokoa mpira na kumkuta mfungaji.

Matokeo hayo yanaifanya Simba kuambulia pointi 1 tu katika michezo yake miwili iliyopita ikitoka sare na Mtibwa na kupoteza leo dhidi ya Azam na kutoa mwanya kwa Yanga kuweza kuongoza ligi kama itashinda kesho dhidi ya Mwadui kwani Simba inabaki na pointi 45 Yanga wakiwa na pointi 43 na Azam wanafikisha pointi 34 katika nafasi ya 4.

Mbio za Ubingwa kwa Simba sasa zitategemea zaidi Yanga kufungwa huku ikitakiwa kushinda mechi zake zilizobaki.


No comments

Powered by Blogger.