MAJANGA : LIVERPOOL YAPIGWA TENA ANFIELD, YAPOTEZA KOMBE LA PILI MSIMU HUU

Ndoto ya mashabiki wa Liverpool kuona timu yao ikishinda ubingwa wa kombe la chama cha soka nchini England FA zimefutika baada ya timu yao kukubayaokichapo cha bao 2-1



Liverpool ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani ilikubali kichapo hicho toka kwa timu ya daraja la kwanza (Championship) Wolves

Dakika ya kwanza tu Liverpool ilishakubali kufungwa bao la kwanza kupitia kwa beki Richard Sterman kisha kufungwa bao la pili dakika ya 41 likifungwa na Andreas Weiman huku Liverpool wakipata bao la kusawazisha dakika ya 86 likifungwa na Divock Origi.

Matokeo hayo yanawafanya Liverpool kutupwa nje ya michuano hiyo ikiwa ni michuano ya pili msimu huu baada ya ile ya kombe la ligi EFL na sasa wanaelekeza nguvu zao katika mechi ya Jumanne dhidi ya Chelsea.

No comments

Powered by Blogger.