MTIBWA VS SIMBA LEO : HAYA NDIYO MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUYAFAHAMU


Vinara wa ligi kuu Tanzania bara Wekundu wa Msimbazi Simba leo watakua katika dimba la Jamhuri mkoani Morogoro kucheza dhidi ya wenyeji Mtibwa Sugar toka Manungu.

Mchezo huo ni mmoja kati ya michezo miwili itakayochezwa leo mwingine ukiwa dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Azam Complex.

www.wapendasoka.com Imekuandalia mambo muhimu usiyoyajua au kama unayajua basi tunakukumbusha kuhusu mchezo huo wa leo huko Mkoani Morogoro.

● Simba wataingia katika mchezo wa leo wakiwa ndiyo vinara wa ligi hiyo wakiwa na pointi 44 huku Mtibwa Sugar wao wakiwa na pointi 30 katika nafasi ya 5.

● Mechi iliyopita baina ya timu hizo Simba iliweza kuibuka na ushindi wa bao 2-0 magoli ya Laudit Mavugo na Ibrahim Ajib mechi ikipigwa Dar es Salaam tarehe 11 Septemba mwaka jana.

● Katika mechi 5 zilizopita kwenye ligi kuu Tanzania bara Simba imeshinda mechi 3 na kufungwa mechi 2 wakati Mtibwa wao wameshinda mechi 4 na kutoka sare mechi moja.

● Kwenye hizo mechi 5 zilizopita Mtibwa Sugar imefanikiwa kufunga magoli 8 na kuruhusu kufungwa goli 3 wakati Simba wao wamefunga goli 5 na kuruhusu kufungwa mara 3.

● Katika mechi 5 zilizopita baina ya timu hizo Simba wameibuka na ushindi mara 4 huku mechi moja tu ikiisha kwa sare wakati Mtibwa hawajawahi kushinda mechi yoyote katika hizo 5 kwenye ligi kuu Tanzania bara.

● Shiza Kichuya mchezaji wa zamani wa Mtibwa ndiye anayeongoza kupachika mabao akifungana na Amiss Tambwe na Simon Msuva wote wakiwa na magoli 9.

No comments

Powered by Blogger.