MAN UNITED YAMPONZA MWAMUZI LIGI KUU ENGLAND, ASHUSHWA DARAJA
Moja ya sababu zilizomshusha daraja mwamuzi huyo anayesifika kwa kutoa kadi nyekundu ni maamuzi mabovu katika mchezo wa ligi kuu nchini humo baina ya West Ham na Manchestekupelekw na Man United kuibuka na ushindi wa bao 2-0.
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la London park mwamuzi huyo alimpa kadi nyekundu kimakosa Mchezaji wa West Ham Sofiane Feghouli na kukubali goli la Zlatan Ibrahimovic ambaye alikua ameotea.
Maamuzi yake ya kutomtoa nje Ross Barkley alipomchezea rafu mbaya Jordan Henderson katika mchezo wa Everton dhidi ya Liverpool pia yamechangia.
Mwamuzi huyo mwenye miaka 48 atatakiwa kuchezesha sasa Dabi ya Yorkshire kati ya Barnsley na Leeds siku ya Jumamosi katika ligi daraja la kwanza na kutolewa kabisa katika ratiba ya waamuzi watakaochezesha ligi kuu weekend hii huku ikisemekana adhabu hii itakua na kwa mechi za weekend hii pekee.
No comments