MAN UNITED YAJIWEKA VIZURI KUTINGA FAINALI KOMBE LA LIGI ENGLAND
Manchester United jana usiku ilijiwekea mazingira mazuri ya kutinga katika fainali ya michuano ya kombe la ligi nchini England kwndkuifunga Hull City bao 2-0.
Mchezo huo ni wa nusu fainali ya kwanza baina ya timu hizo huku mechi ya marudiano ikipangwa kufanyika baada ya wiki mbili ambapo mshindi wa jumla atatinga katika fainali dhidi ya Liverpool au Southampton.
Juan Mata alitangulia kuipatia United bao la kwanza kipindi cha pili baada ya kumaliza kipindi cha kwanza matokeo yakiwa ni sare ya bila kufungana huku Maruane Fellaini akifunga bao la pili lililohakikishia ushindi kwa Man United katika dimba la Old Trafford.

No comments