MAKELELE AREJEA LIGI KUU YA ENGLAND

Kocha mpya wa Swsnsea City inayoshiriki ligi kuu nchini England Paul Clement amesmua kumjumuisha kiungo wa zamani wa Ufaransa na klabu ya Chelsea Claude Makelele.

Clement ambaye alikua msaidizi wa Kocha Carlo Ancellot akiwa na Makelele pia wakati wakiwa PSG amemjumuisha Makelele katika benchi lake la ufundi katika harakati za kuweza kuibakiza Swansea Ligi kuu.

Makelele mwenye miaka 43 hivi sasa amesaini mkataba wa kuwa katika benchi la ufundi mpaka mwisho wa msimu huu.


No comments

Powered by Blogger.