MACHO YOTE ENGLAND LEO NI MAN CITY VS TOTTENHAM: RATIBA KAMILI HII HAPA
Ligi kuu ya soka ya England maarufu kama EPL inaingia hatua yake ya 22 leo kwa michezo 7 kupigwa katika viwanja 7 tofauti nchini humo.
Macho na masikio yatakua katika uwanja wa Etihadi Jijini Manchester katika mechi ya mwisho hii leo majira ya saa 2 na nusu kwa saa za hapa nyumbani wakati Manchester City chini ya Pep Guadiola watakapoikaribisha Tottenham Hotspurs chini ya Mauricio Pochettino.
Tottenham inakamata nafasi ya pili ikiwa na pointi 45 sawa na Liverpool lakini Spurs wana uwiano mzuri ws magoli ya kufunga na kufungwa wakati Manchester City ambayo msimu ulipoanza wengi waliipa nafasi ya kuchukua ubingwa inakamata nafasi ya 5 ikiwa na pointi 42.
Sambamba na mechi hiyo Stoke City watakua nyumbani kuwaalika mashetani wekundu Manchester United huku Stoke ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kupata sare katika mechi ya awali pale Old Trafford.
Mapema kabisa hii leo Liverpool wakiwa nyumbani wataialika Swansea City inayopigania kutoshuka daraja mchezo ambao ni muhimu kwa timu zote.
HII HAPA RATIBA KAMILI KWA SAA ZA HAPA NYUMBANI
● Saa Tisa na Nusu Alasiri
- Liverpool vs Swansea
● Saa 12 Jioni
- AFC Bournemouth vs Watford
- Crystal Palace vs Everton
- Middlesbrough vs West Ham United
- Stoke City vs Manchester United
- West Brom vs Sunderland
● Saa 2 na nusu Usiku
- Manchester City vs Tottenham Hotspur

No comments