AFCON 2017: SARE DHIDI YA CONGO YAWAWEKA PABAYA MABINGWA WATETEZI IVORY COAST.
Michuano ya kombe la mataifa ya Afrika Afcon 2017 iliendelea jana kwa mechi 2 za kundi C kuchezwa katika viwanja viwili tofauti nchini Gabon.
Mabingwa watetezi wa kombe hilo Ivory Coast kwa mara ya pili mfululizo waliweza tena kutoka sare ya bao 2-2 na Congo DR ukiwa ni mchezo wa awali hiyo jana.
Neeelskens Kebano alitangulia kuipatia Congo bao la kwanza dakika ya 10 tu ya mchezo kabla ya Wilfried Bonny hajaisawazishia Ivory Coast lakini Junior Kabananga aliihakikishia Congo kwenda mapumziko ikiwa mbabe.
Kipindi cha pili nguvu ya ziada ilitumika pamoja na uzoefu kuweza kupata bao la kusawazisha kwa Ivory Coast likifungwa na Serey Die na kufanya mabingwa hao watetezi kuambulia pointi 1 kama ilivyokua katika mechi ya awali.
Katika mechi ya pili hiyo jana Morocco waliweza kuifunga Togo kwa bao 3-1 magoli ya Aziz Bouhaddouz, Roman Saiss na Youssef En-Nesryi huku Togo chini ya nahodha Emmanuel Adebayor ikipata goli la kufutia machozi lililowekwa kimiani na Methieu Dossevi.
Matokeo ya mechi za jana yanaifanya Congo kuongoza kundi ikiwa na pointi 4 Morocco wanafatia wakiwa na pointi 3 wakati Ivory Coast wana pointi 2 na Togo wakiwa na pointi yao 1 na kufanya michezo ya mwisho ya kundi hilo itakayopigwa wiki ijayo kuamua timu zipi zitafuzu.

No comments