LIVERPOOL YAKUMBANA NA KICHAPO TOKA KWA SOTON KOMBE LA LIGI

Mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya pili ya kombe la Ligi nchini England (Zamani Capital One) baina ya wenyeji Southampton na Liverpool umemalizikaakwa Southampton kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Mechi hiyo iliyochezwa katika dimba la St. Marrys Ilishuhudia Liverpool ikifungwa bao pekee dakika ya 20 na mshambuliaji Nathan Redmond.

Kama si ushujaa wa kipa wa Liverpool Loris Karius kuokoa michomo kadhaa ya washambuliaji wa Southampton basi magoli yangeweza kuwa zaidi ya 1-0

Hii ni mechi ya kwanza baina ya timu hizo katika hatua ya nusu fainali huku mechi ya  marudiano ikitarajiwa kupigwa majuma mawili yajayo katika dimba la Anfield ambapo mshindi wa jumla ndiye atacheza fainali dhidi ya Manchester United au Hull City.

No comments

Powered by Blogger.