AJIBU AREJEA SIMBA IKIPOKWA POINTI NA MTIBWA SUGAR MOROGORO
Vinara wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Wekundu wa msimbazi Simba wameshindwa kupata matokeo ya ushindi katika mechi yake ya jioni hiI dhidi ya Mtibwa sugar
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Jamhuri mjini Morogoro haukuwa na ufundi wowote baada ya uwanja huo kuonekana hauko katika hali nzuri
Licha ya kosakosa nyingi za Simba kipindi cha kwanza kupitia kwa washambuliaji wake Laudit Mavugo na Juma Luizio lakini ngome ya Mtibwa ilikuwa Imara chini ya uongozi wa mkongwe Shaaban Nditi
Katika mchezo huo Simba ilimkaribisha kikosini kwa mara ya kwanza baada ya kuwa nje ya kikosi kwa muda mrefu mshambuliaji Ibrahim Ajib aliyekua nje ya nchi kwa majaribio ya kucheza soka la kulipwa akiingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Laudit Mavugo
Kwa matokeo hayo Simba imepunguza wigo wa pointi dhidi ya Yanga kufikia pointi mbili Simba Ikiongoza ligi ikiwa na pointi 45 huku Mtibwa wakipanda mpaka nafasi ya 4 na pointi zao 31.

No comments