AFCON 2016 : WENYEJI GABON HALI MBAYA, CAMEROON YAPATA USHINDI WA KWANZA

Mechi za mzunguko wa pili wa kombe la mataifa ya Afrika AFCON 2016 hatua ya makundi zilianza kupigwa usiku wa jana kwa timu nne za kundi A kucheza.


Wenyeji Gabon kwa mara nyingine walishindwa kupata ushindi katika michuano hiyo baada ya kuambulia sare tena ya bao 1-1 na Bukina Faso.

Mchezaji wa Bukina Faso Prejuce Nakuolma aliyeingia dakika ya 11 baada ya kuumia Jonathan Pitroita alifunga bao la kuongoza kwa Bukina Faso kabla ya nahodha wa Gabon Pierre Emerick-Aubameyang hajaisawazishia Gabon kwa bao la penati.

Hii ni sare ya pili kwa Gabon ambao walitoka sare kama hiyo na Guinne Bissau katika mechi ya ufunguzi.

Katika mechi nyingine hiyo jana Cameroon waliweza kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Guinea-Bissau mabao ya Cameroon yakifungwa na Sebastian Siani na Michael Ngadeu-Ngadjui baada ya Guinea-Bissau kutangulia kufunga kupitia kwa Piqueti

RATIBA YA LEO

● Algeria vs Tunisia (Saa 1 Jioni)
● Zimbabwe vs Senegal (Saa 4 Usiku)


No comments

Powered by Blogger.