YAMETIMIA: KOCHA WA KWANZA ATIMULIWA MSIMU HUU LIGI KUU YA ENGLAND


Ule msemo wa makocha wanaajiriwa ili kufukuzwa unaendelea kuleta maana baada ya leo kushuhudia kocha wa kwanza msimu huu akifukuzwa katika timu zinazoshiriki ligi kuu ya England.

Allan Pardew mchezaji wa zamani wa Crystal Palace na mmoja wa makocha walioweka historia katika klabu ya Crystal Palace amefukuzwa kuinoa klabu hiyo yenye maskani yake jijini London.

Pardew anatimuliwa na Crystal Palace wakati huu klabu hiyo ikishika nafasi ya 17 katika msimamo wa ligi hiyo maarufu duniani.

Pardew aliteuliwa kuifunza Palace mwezi Januari mwaka 2015 na kufanikiwa kuisaidia klabu hiyo kumaliza ndani ya timu 10 bora msimu ulipomazika licha ya kuikuta klabu katika hatari ya kushuka daraja kutokana na matokeo mabovu lakini ameshindwa kuonyesha makali yake msimu huu akishinda mechi moja tu katika mfululizo wa mechi 11.

Tayari jina la Sam Alladyce kocha wa zamani wa England aliyetimuliwa baada ya kashfa linatajwa kati ya watu wanaopewa nafasi kubwa kumrithi  Pardew.

No comments

Powered by Blogger.