SADIO MANE AIPA LIVERPOOL USHINDI DAKIKA YA MWISHO


Mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal anayeichezea Liverpool Sadio Mane jana Usiku aliibuka shujaa wa timu yake katika mechi ya Wapinzani wa jadi wa jiji la Liverpool.

Mane alifunga bao pekee katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Goodson Park dhidi ya wenyeji Everton.

Dakika ya 5 ya muda wa nyongeza shuti lililopigwa na Daniel Sturadge liligonga mwamba ndipo Sadio Mane akamalizia na kuwapa Liverpool ushindi muhimu katika harakati za kutafuta nafasi ya kutwaa ubingwa.


No comments

Powered by Blogger.