HII NDIYO TOFAUTI YA MESSI NA RONALDO TANGU RONALDO ALIPOJIUNGA NA REAL MADRID
Tumebahatika kuishi katika nyakati ambazo tunawashuhudia wachezaji wawili bora zaidi kuwahi kutokea duniani yani Cristiano Ronaldo nahodha wa Ureno na mshambuliaji wa mabingwa wa Ulaya na dunia Real Madrid na mwenzake Lionel Messi ambaye ni nahodha wa Argentina na mshambuliaji wa Mabingwa wa Spain Barcelona.
Tangu Real Madrid walipovunja rekodi ya uhamisho kwa kumsajili Cristiano Ronaldo toka Manchester United kumeibuka ushindani mkubwa ndani ya Spain na katika ulimwengu wa Wapenda Soka kuhusu nani bora kati ya hawa wachezaji wawili.
Uwezo wao mkubwa wa kufunga unawafanya wachezaji hawa kuwa katika 'level' nyingine huku wakivunja rekodi kila kukicha.
Ni ngumu kusema nani mkali kuzidi mwenzake nami Leo nimekuandalia baadhi ya mambo ambayo yamefanywa na wawili hawa tangu mwaka 2009 ambao Ronaldo ndipo alipojiunga na Real Madrid.
● Wakali hao kila mmoja ameshafunga magoli 270 kwenye ligi kuu ya Spain La Liga mpaka sasa na hii ni tangu mwaka 2009.
● Magoli hayo hapo juu Cristiano Ronaldo amefanikiwa kufunga katika michezo 247 ya La Liga huku Lionel Messi yeye akifunga magoli hayo katika michezo 252 aliyocheza katika La Liga.
● Katika mechi hizo hapo juu Lionel Messi ameibuka kinara katika kutoa Pasi za magoli (Assists) akiwa ameshafanya hivyo mara 104 wakati Ronaldo yeye ametoa Assists 78 katika mechi hizo za La Liga.
● Tangu mwaka 2009 Cristiano Ronaldo amefanikiwa kufunga magoli 380 katika mechi 367 huku Lionel Messi akifunga magoli 396 katika mechi 390 na hii ni katika mashindano yote katika klabu zao.
● Kwa upande wa mataji waliyoshinda Tangu mwaka 2009 Messi ameshinda Ubingwa wa La liga mara 5, Copa Del Ray mara 3 na ubingwa wa Ligi ya mabingwa Ulaya mara 2.
Ronaldo yeye tangu mwaka 2009 ameshinda Ubingwa wa ligi kuu ya Spain La Liga mara 1, Copa Del Rey mara 2 na ubingwa wa Ligi ya mabingwa Ulaya mara 2.
● Cristiano Ronaldo amefunga magoli matatu au zaidi katika mechi (Hat-trick) mara 40 wakati Lionel Messi amefanya hivyo mara 37 wakiwa na klabu zao tangu maka 2009.
● Cristiano Ronaldo amefunga magoli matatu au zaidi katika mechi (Hat-trick) mara 40 wakati Lionel Messi amefanya hivyo mara 37 wakiwa na klabu zao tangu maka 2009.
Kwa Leo naomba niishie hapa ila kuna Rekodi Nyingi zaidi hawa watu wameshaziweka nitazileta siku nyingine.
By Edo DC
Kwa maoni nicheki
Kwa maoni nicheki
Instagram @Edodanielchibo
Twitter: EdoDaniel1
Email: wapendasoka@gmail.com
Twitter: EdoDaniel1
Email: wapendasoka@gmail.com
No comments