LIGI KUU TANZANIA BARA LEO NAFASI YA SIMBA KUIKIMBIA YANGA,AZAM KUJIULIZA KWA MAJIMAJI


Mechi za pili za mzunguko wa pili katika ligi kuu ya Soka Tanzania bara zinaendelea leo baada ya jana mchezo pekee uliopigwa katika dimba la Uhuru kumalizika kwa sare ya bao 1-1 kati ya wenyeji African Lyon na mabingwa watetezi Yanga.

Vinara wa ligi hiyo Wekundu wa Msimbazi Simba leo watakua uwanja wa Uhuru kuwaalika JKT Ruvu kwenye mechi ambayo Simba inahitaji ushindi ili kuongeza wigo wa pointi katika harakati za kuwania ubingwa msimu huu.

Simba ina pointi 38 katika nafasi ya kwanza pointi moja mbele ya Yanga na ushindi katika mechi ya leo utaleta matumaini ya kutwaa ubingwa.

Azam FC baada ya kulazimishwa sare wiki iliyopita leo itakua mkoani Ruvuma kucheza na Wenyeji Maji Maji ya huko.

Mbao FC ya Mwanza itakua itakua ugenini kucheza na Mwadui, wakati Mbeya City wakiwaalika Toto Africans  huku Kagera Sugar wakiwaalika Stand United katika dimba la Kaitaba na Ndanda FC wataialika Mtibwa Sugar.


No comments

Powered by Blogger.