HII HAPA RATIBA YA MECHI ZA LEO NA MATOKEO YA MECHI ZA JANA LIGI KUU TANZANIA BARA
Wekundu wa msimbazi Simba wanaanza kampeni yao ya kuwania ubingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania bara mzunguko wa pili kwa kuwakabili Ndanda FC toka mkoani Mtwara mechi itakayofanyika katika dimba la Nangwanda mjini Mtwara.
Simba ambayo ilinyanyasa mzunguko wa kwanza kwa kumaliza kama vinara wa ligi hiyo sasa inataka kuendeleza wimbi la ushindi iliyojulikana Kufufua matumaini ya kushinda ubingwa msimu huu.
Tayari Yanga imefikisha pointi 36 pointi moja zaidi ya Simba na ushindi pekee utawarudisha Simba katika uongozi wa ligi hiyo.
RATIBA KAMILI YA MECHI ZA LEO
● Ndanda FC vs Simba SC
● African Lyon vs Azam FC
● Mbao FC vs Stand United
● Prisons vs Majimaji
MATOKEO YA MECHI ZA JANA
○ JKT Ruvu 0-3 Yanga SC
○ Ruvu Shooting 1-1 Mtibwa Sugar
○ Mbeya City 0-0 Kagera Sugar
○ Mwadui FC 1-0 Toto Africans
1090
ReplyDelete13 90
ReplyDelete