SIMBA YARUDI KILELENI LIGI KUU TANZANIA BARA,AZAM YAANZA NA SARE
![]() |
Picha toka maktaba |
Mchezo huo wa kwanza kwa timu hizo katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo ulichezwa katika dimba la Nangwanda Mjini Mtwara.
Magoli ya Simba yaliwekwa kimiani na Mzamiru Yasin na Mohamed Ibrahim katika mchezo ambao Simba ilihitaji ushindi ili kuweza kurudi kileleni baada ya jana Yanga kushinda bao 3-0 dhidi ya JKT Ruvu.
Katika mchezo mwingine hii leo Azam FC walitoka sare ya bila kufungana na African Lyon mchezo uliopigwa katika dimba la Uhuru.
Huko jijini Mwanza wenyeji Mbao FC waliweza kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Stand ya Shinyanga.
Prisons ikiwa nyumbani imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Majimaji FC toka Songea
Baada ya matokeo ya leo Simba wanafikisha pointi 38 katika nafasi ya kwanza wakifatiwa na Yanga wenye pointi 36 huku Toto Africa wakishika mkia na pointi zao 12.
No comments