FA WAIPIGA CHINI RUFAA YA VARDY.

Mshambuliaji wa Leicester City Jamie Vardy atatumikia adhabu ya kadi nyekundu kwa kukosa michezo mitatu baada ya chama cha soka cha England, FA kukataa rufaa yake.

Vardy alioneshwa kadi nyekundu baada ya kuonekana amemchezea madhambi Mame Diouf wa Stoke City katika mchezo ambao walitoka sare ya 2-2  jumamosi iliyopita.

Leicester hawakuridhika na maamuzi hayo hivyo wakaamua kukata rufaa lakini FA wamemkuta Vardy na hatia na hivyo kuibariki adhabu yake.

No comments

Powered by Blogger.