DROO LIGI YA MABINGWA AFRIKA IMEKAMILIKA, WAPINZANI WA YANGA HADHARANI

Shirikisho la soka barani Afrika leo limeendesha droo ya ligi ya mabingwa barani Afrika ambayo inataraji kuanza kutimua vumbi mapema mwakani.

Wawakilishi wa Tanzania bara, Yanga wanataraji kuanza kampeni hiyo katika hatua ya mtoano kwa kuwavaa mabingwa wa Comoro
Ngaya De Mbe huku Yanga wakianzia ugenini.

Michuano hiyo itaanza mwezi Februari 2017 kwa michezo ya kwanza kuchezwa kati ya tarehe 10,11 na 12 na michezo ya marudiano itachezwa kati ya tarehe 17,18 na 19.

No comments

Powered by Blogger.