BARCELONA NA REAL MADRID KATIKA MTIHANI MZITO KOMBE LA MFALME. RATIBA HII HAPA
Droo ya hatua ya 16 bora katika michuano ya kombe la Mfalme nchini Spain Maarufu kamma Copa Del Rey imepangwa jana Ijumaa huku Barcelona na Real Madrid wakipangwa na timu ngumu hatua hii.
Mabingwa watetezi wa kombe hilo klabu ya Barcelona ambayo ndiyo klabu inayoongoza kwa kulitwaa kombe hilo mara 28 ikipangwa kucheza dhidi ya Athletic Bilbao mechi ya kwanza Barca wakianzia Ugenini.
Real Madrid kwa upande wao wamepangwa kukutana na Sevilla ambao msimu uliopita walifika fainali na kupoteza dhidi ya Barcelona.
Utaratibu wa michuano hiyo hufanyika kwa mtindo wa mechi za nyumbani na ugenini kuaniz mechi ya kwanza mpaka fainali.
Ratiba nyingine ni kama inavyoonekana katika picha
Hatua ya 16 bora itachezwa tarehe 4 Januari 2017 na marudio yake ni tarehe 11 Januari 2017
No comments