YANGA WAONDOKA NA POINTI TATU MUHIMU MBEYA
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara Yanga leo wamefanikiwa kuondoka na pointi tatu katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya baada ya kuwanyamazisha Tanzania Prisons kwa bao 1-0.
Bao la Yanga katika mchezo huo lilipatikana katika dakika ya 74 ya mchezo kwa njia ya mkwaju wa penati uliopigwa na Saimon Msuva baada ya yeye mwenyewe kuchezewa madhambi katika eneo la hatari.
Mchezo ulitawaliwa na rabsha za hapa na pale, matumizi ya nguvu lakini pia haukukosa ufundi hasa katika eneo la kiungo ambapo kila timu ilijidhatiti vilivyo kuhakikisha inaibuka na ushindi.
Itakua ni siku nzuri sana kwa golikipa wa Yanga Beno Kakolanya ambaye aliiokoa timu yake kwa kupangua mkwaju wa penalt mapema kipindi cha pili.
Kwa matokeo hayo, Yanga wamefikisha pointi 30 wakiwa nyuma ya Simba inayoongoza kwa tofauti ya pointi 5

No comments