WAPENDA SOKA FC YAIBUKA NA USHINDI MECHI YA KIRAFIKI DAR

Vonso Almeida akifunga bao la pili 
Mchezo wa kirafiki wa soka kati ya timu ya Taasisi ya Wapenda soka Tanzania ambao ni wamiliki wa mtandao huu ambayo ilikua ikicheza na timu ya kampuni ya Printing umemalizika kwyaushindi wa bao 2-1 kwa Wapenda soka FC.

Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa shule ya sekondari ya Wasichana ya Zanaki Hapa Jijini leo jioni ulikua mkali huku kipa wa timu ya Printers FC Dau Juma akionekana ndiye shujaa wa mchezo huo baada ya kuokoa mashuti 7 yaliyopigwa langoni mwake kipindi cha kwanza.

Shuti pekee lililopigwa na Printers FC dakika ya 36 lilizaa goli pekee kwa timu hiyo lililofungwa na Ally Sella baada ya kuihadaa safu ya ulinzi Wapenda Soka FC iliyokua ikiongozwa na nahodha Nick Emma,Godlisten Anderson Chicharito na Noel Ndidi na kupiga shuti kali lililomshinda kipa Edo DC.

Mpaka mapumziko Wapenda Soka FC ilikua nyuma kwa bao hilo moja licha ya jitihada kubwa za safu ya ushambuliaji iliyokua ikiongozwa na Humphrey Mrope, Jackah na Vonso Almeida.

Kipindi cha pili Mabadiliko ya kumtoa Jackah na kuingia Musa Kimangale "Moki" yaliongeza nguvu kwa Wapenda Soka FC baada ya kufanya mashambulizi ya mara kwa mara na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha likifungwa na winga Abuu Kim baada ya kupiga shuti kali lililomzidi kipa Dau Juma.

Baada ya bao hilo Wapenda Soka FC iliongeza mashambulizi na kazi nzuri ya Men Lufu Mbawala kuwapiga chenga mabeki kadhaa na kumtangulizia Vonso Almeida ilizaa goli la pili dakika ya 76 ya Mchezo Likifungwa na Vonso aliyekua akishambulia kutokea winga ya kulia.

Baada ya mchezo huo Wapenda Soka FC inaendelea na mazoezi na kujiandaa na mchezo mwingine utakaopigwa mwishoni mwa mwezi huu.

No comments

Powered by Blogger.