MIWANI PANA YA EDO DC: KUTANA NA RB LEIPZIG INAYOKIMBIZA BUNDESLIGA IKIWA NA MCHEZAJI WA 'KITANZANIA'
RasenBallsport Leipzig ikijulikana kwa kifupi kama RB Leipzig jina geni katika soka la Ujerumani ikipanda daraja la Bundesliga msimu huu tayari imeanza kuzinyanyasa klabu kongwe zinazoshiriki ligi hiyo inayoaminiwa ni ngumu zaidi kushiriki.
Klabu hii ilianzishwa rasmi mwaka 2009 na uanzishwaji wake ulitokana na miaka takribani mitatu ya juhudi kubwa za uwekezaji katika soka wa kampuni ya kutengeza vinywaji (Energy drink) Red Bull GmbH ya nchini Ujerumani kugonga mwamba katika vilabu mbalimbali.
Kampuni ya Red Bull GmbH walitaka kuwekeza pesa nyingi katika soka kwa kununua vilabu vikongwe kama FC Sachsen Leipzig, 1860 Munich na ST. Pauli ili kujitangaza zaidi kibiashara lakini mpango wao ulikumbwa na changamoto nyingi hasa kushindwa kukubaliwa na kupata upinzani mkali toka kwa mashabiki wa vilabu hivyo waliokua wakipinga hoja ya mabadiliko ya kuuzwa kwa klabu husika.
Mwaka 2009 kampuni hiyo ilifanikiwa kuinunua klabu ya daraja la 5 nchini Ujerumani SSV Markranstädt lengo likiwa ni moja tu kuifikisha klabu hiyo katika hatua ya juu ya soka la Ujerumani ndani ya miaka 8 na sasa lengo hilo limetimia baada ya kupanda daraja msimu huu.
Red Bull Arena ndiyo uwanja wa nyumbani wa Leipzig klabu ambayo tangu imenunuliwa na wawekezaji hao wakubwa imekua ikipanda daraja moja baada ya lingine mpaka kufika katika Bundesliga na tofauti na timu nyingi zinazopanda daraja RB Leipzig inakimbizana na Bayern Munich pale juu katika msimamo wa Bundesliga zote zikiwa na pointi 24 japo Bayern wana faida ya magoli mengi ikiwaacha wakongwe Borussia Dortmund,Bayer Leverkusen n.k
RB Leipzig inakuwa timu ya 5 kumilikiwa na kampuni ya vinywaji vya Red Bull japokuwa nchini Ujerumani pekee wameshindwa kubadili jina na kuingiza jina la Red Bull kutokana na chama cha soka cha Ujerumani kugomea kutumia jina la kampuni nataka ujue pia kwamba Kampuni ya Red Bull inamiliki timu nyingine kadhaa duniani zijiwemo FC Red Bull Salzburg ya Austria,New York Red Bulls ya Marekani,Red Bull Brasilin ya Brazil na Red Bull Ghana ya Ghana.
Kwa taarifa yako tu ni kwamba Kuna damu ya Kitanzania inayoaminiwa katika timu hii linapokuja swala la kupachika mabao nayo si mwingine ni Mshambuliaji Yusuf Poulsen mwenye Uraia wa Denmark lakini mama yake mzazi ni Mwenyeji wa Tanga.
Yusuf aliamua kuchukua uraia wa Denmark baada ya kulelewa na kukulia huko na baba yale alifariki wakati akiwa na miaka 6 tu.
Kwa kifupi tu hii ndiyo RB Leipzig ambayo haijapoteza mchezo wowote katika Bundesliga msimu huu na wale wataalamu wa kubeti tayari wananufaika na kuiwekea "Mzigo" timu hii na swali ni je wataweza kuendeleza huu moto waliouanzisha?
Imeandaliwa na Edo DC
Email: wapendasoka@gmail.com
Instagram: @edodc

![]() |
Yussuf Poulsen |

No comments