WAGENI RB LEIPZIG WASHIKA USUKANI BUNDESLIGA
Timu ngeni katika ligi kuu nchini Ujerumani Bundesliga RB Leipzig imeendeleza makali yake baada ya kuifunga Bayer Leverkusen bao 3-2 ugenini usiku wa jana.
Ikicheza nyumbani Leverkusen ilikua ya kwanza kupata bao la kwanza likifungwa na Kevin Kampl dakika ya kwanza tu ya mchezo kabla ya Leipzig hawajasawazisha kwa goli la kujifunga la beki Julian Baumgartlinger.
Julian Brandt aliifungia Leverkusen bao la pili dakika moja kabla ya mapumziko lakini kipindi cha pili RB Leipzig walucharuka na kusawazisha bao hilo kupitia kwa Emil Forsberg na kisha kapteni wa RB Leipzig Willi Orban akafunga bao la ushindi.

Kwa matokeo hayo Leipzig inakwea kileleni mwa msimamo wa ligi ikifikisha pointi 27 ikiwa ni pointi 3 mbele ya Bayern Munich ambao leo wanacheza na Borussia Dortmund.
No comments