VAN PERSE AREJEA DIMBANI NA KUISAIDIA FERNEBAHCE KUIMALIZA GALATASARAY
Robin Van Perse ameingia katika historia ya kuwa mchezaji anayefunga katika kila mechi zinazohusisha timu pinzani za mji mmoja (derby) baada ya kufunga bao 2 katika derby ya Kitalararasi jijini Instabul Uturuki.
Fernebahce iliweza kushinda mechi hiyo kwa ushindi huo wa bao 2-0 dhidi ya Galatasaray katika moja kati ya michezo iliyotikisa vichwa vya habari barani Ulaya wikiend hii.
Robin Van Perse alirejea dimbani baada ya ajali iliyohusisha kuumia vibaya kwa jicho lake katika mchezo uliopita wa ligi hiyo ya Uturuki hali iliyopelekea kuzushwa kwamba mchezaji huyo asingeweza kuona tena lakini Amepona na jana alikua 'fit' kuiongoza Fernebahce katika mechi hiyo muhimu.

Van Perse alifunga goli moja kila kipindi la kwanza akimalizia mpira wa krosi ya Sener huku la pili akilifunga kwa njia ya penati kipindi cha pili.
Kwa magoli hayo Robin Van Perse sasa ameweza kufunga magoli katika Derby kubwa zote alizocheza akifunga dhidi ya Ajax wakati yuko Feyernood,akaifungia Arsenal dhidi ya Tottenham na baadae akaifungia Manchester United dhidi ya Manchester City.
Fernebahce inapanda mpaka nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi hiyo ikifikisha pointi 21 ikiwa ni pointi 6 nyuma ya vinara Besiktas
No comments