DABI YA MILAN HAKUNA MBABE, SUSO AIBEBA AC MILAN
![]() |
Suso akishangilia moja ya mabao yake |
Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 2-2 AC Milan wakitangulia kupata bao la uongozi dakika ya 42 likifungwa na mchezaji wa zamani wa Liverpool Suso ambaye alifunga mabao yote mawili kwa AC Milan.
Magoli ya Inter Milan yalifungwa na Antonio Candreva na Ivan Perisic ambaye alifunga dakika za lala salama kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare hiyo ya bao 2-2.
AC Milan wanashika nafasi ya 3 wakiwa na pointi 26 wakati Inter Milan inashika nafasi ya 9 na pointi zao 18 katika msimamo wa ligi kuu ya Italia Serie A inayoongozwa na Juventus yenye pointi 33.
No comments