RUVU SHOOTING WAIANGUKIA TFF MECHI YAO NA YANGA ISOGEZWE MBELE.
Uongozi wa timu ya Ruvu Shooting ya Pwani umeiandikia barua Bodi ya Ligi/TFF kuiomba isogeze mbele mchezo wao dhidi ya Yanga uliopangwa kufanyika November 9, 2016 hadi timu ya Taifa itakaporejea kutoka Zimbabwe.
Afisa habari wa Ruvu Shooting alisema,
"Tumepeleka maombi hayo Bodi ya Ligi/TFF kutokana na hali ya usafiri na uchovu kwa wachezaji ambao tunawategemea kuwasili Mlandizi kesho Jumanne saa 1.42 asubuhi wakitokea Bukoba kwenye mchezo wa ligi uliochezwa jana November 6, 2016 katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba." Amesema Masau.
"Kutoka Bukoba hadi Kibaha ni umbali wa KM 1,450 . Kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani, mwendo wa gari unatakiwa uwe KM 80 kwa saa, kwa maeneo yasiyo makazi ya watu na KM 50 kwa saa, kwa maeneo ya makazi ya watu. Kwa wastani gari lililowabeba wachezaji wetu ambalo liko njiani mpaka sasa, linakwenda mwendo wa KM 65 kwa saa."
Masau aliongeza kwa kutanabaisha kuwa Kwa mwendo huo, yatahitajika masaa 22 na dakika 18 ili kukamilisha safari hiyo ndefu ya kutoka Bukoba hadi Kibaha, Mlandizi.
Mchezo huu awali ulipangwa uchezwe November 10, lakini kwa mujibu wa Masau ni kwamba waliandika barua ya maombi kwa Bodi ya Ligi/TFF kuomba usogezwe mbele ambapo Bodi ya Ligi/TFF waliliona hilo wakafafanya mabadiliko ya mchezo huo kutoka November 10 hadi November 11.
"Lakini siku chache baadaye, Bodi ya Ligi/TFF walifanya mabadiliko mengine kuhusu siku ya mchezo huo, kutoka November 11 kurudi November 10 na baadaye tena wamefanya mabadiliko mengine ya siku ya mchezo huo huo kutoka November 10 hadi November 9!"

No comments