MALINZI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA SIMBA NA BUNGE.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Jamal Emil Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai kutokana na kifo cha Spika Mstaafu wa bunge
hilo la Tanzania, Samwel Sitta.
Mzee Sitta ambaye ni Mbunge wa zamani wa Jimbo la
Urambo lililopo mkoani Tabora amefariki dunia usiku wa kuamkia jana Novemba 7,
2016 kwenye Hospitali ya Chuo Kikuu cha Technical iliyopo Munich nchini
Ujerumani usiku wa kuamkia leo Novemba 7, 2016.
Rais Malinzi amesema kwamba Sitta ameacha alama ya
ucheshi na upenzi katika michezo hususani soka kwani enzi zake hakuficha
mapenzi yake kwa klabu ya Simba alikokuwa mwanachama.
Salamu za rambirambi za Rais Malinzi zimekwenda pia
kwa Rais wa Klabu ya Simba, Evance Aveva, familia ya marehemu, ndugu, jamaa na
marafiki. Amewataka kuwa watulivu wakati huu mgumu wa kumpoteza Mzee Samwel
Sitta na kwamba anaungana nao kwenye maombolezo
.
Akimwelezea zaidi Mzee Sitta, Rais Malinzi amesema
kwamba "Binafsi nitamkumbuka na kuenzi uchapakazi wake. Alikuwa
Mwanamichezo aliyekuwa na Mzalendo hususani alipokuwa Spika wa Bunge kuanzia
mwaka 2005 hadi mwaka 2010 na alikuwa pia Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba.
Aliwahi kuwa waziri katika wizara mbalimbali kwa vipindi tofauti.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Jina la Bwana Lihimidiwe.
No comments