MOYO WA HURUMA: MESSI AWALIPA MISHAHARA WAFANYAKAZI WA TIMU YA TAIFA YA ARGENTINA
Nahodha wa Argentina na mchezaji bora wa dunia anayeichezea Barcelona ya Spain Lionel Messi alijipa jukumu la kuwalipa mishahara wafanyakazi wa timu ya Taifa ya Argentina.
Messi alionyesha ukarimu huo baada ya wafanyakazi wanaofanya kazi katika kitengo cha ulinzi kumfata na kumpa malalamiko yao kwa kutolipwa mishahara kwa takribani miezi 6 sasa.
Malalamiko ya wafanyakazi hao yaliwasilishwa na mmoja wao kwa Messi ambaye ni kiongozi wa timu kabla ya mechi dhidi ya Brazil ya kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la dunia wakimuomba awasaidie kupata stahiki zao wanazodai katika shirikisho la soka nchini Argentina.
Messi akijua hali ngumu ya kifedha inayolikabili shirikisho la soka nchi Argentina aliamua kumpigia simu baba yake Jorge akimuomba aandae malipo ya wafanyakazi hao swala ambalo lilitekelezwa na baba yake huyo ambaye pia ni mshauri wake mkuu katika kazi yake ya soka.
No comments