BAADA YA USHINDI UGENINI CHELSEA NDIYO VINARA WA LIGI KUU NCHINI ENGLAND


Hatua ya 12 ya ligi kuu ya England iliendelea jioni ya leo Jumapili kwa mechi moja tu kuchezwa baina ya Wageni katika ligi Middlebrough na Chelsea.

Mechi hiyo iliyopigwa katika dimba la River Side ilishuhudia Chelsea ikiibuka na ushindi wa bao 1-0.

Goli pekee katika mchezo huo likifungwa na Diego Costa kipindi cha kwanza goli ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo likiwa ni goli lake la 10 msimu huu katika ligi kuu ya England.

Ushindi huo ni wa 6 mfululizo kwa Chelsea maimu huu katika mechi zote hizo Chelsea haijafungwa goli lolote.

Kwa matokeo hayo Chelsea wanafikisha pointi 28 ikishika usukani wa ligi hiyo8ikifatiwa kwa karibu na Liverpool na Manchester City wenye pointi 27.

No comments

Powered by Blogger.