ISCO AINUSURU SPAIN NA KIPIGO TOKA KWA ENGLAND, ITALY NA UJERUMANI SARE


Pambano la kirafiki kati ya Mabingwa wa zamani wa dunia na Ulaya Timu ya Taifa ya Spain na England lilimalizika kwa sare ya bao 2-2.

Mabao mawili ya dakika za mwisho ya Iago Aspas na Isco yaliwezesha Spain kusswazisha magoli mawili ya England katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Wembley Jijini London.

Adam Lallana alitangulia kuipatia England bao la mapema kabisa kwa njia ya penati baada ya Jamie Vardy kuangushwa na kipa Pepe Reina katika eneo la hatari na mwamuzi kuamuru kupigwa kwa penati hiyo.

Bao la pili la England lilifungwa na Jamie Vardy dakika chache tu baada ya mapumziko ikiwa ni goli lake la kwanza baada ya kucheza dakika 937 bila kufunga kwa klabu na timu ya taifa.

Katika mechi nyingine hiyo jana Italia ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani walilazimishwa sare ya bila kufungana na Ujerumani.

Ufaransa wao wakatoka sare ya bila kufungana na Ivory Coast pambano lililopigwa nchini Romania.



No comments

Powered by Blogger.