EPL : TATHMINI YA MECHI ZA WEEKEND,UNITED YAIBUKIA KWA SWANSEA,CHELSEA NA LIVERPOOL ZATOA VICHAPO VYA NGUVU,ARSENAL, MAN CITY SARE


Ligi kuu Uingereza iliingia katika mzunguko wake wa 11 weekend iliyoisha jana kwa mechi 10 zikipigwa huku kukiwa na jumla ya magoli 36 yaliyofungwa katika mechi zote hizo.


● Liverpool na Chelsea ndizo timu zilizopata magoli mengi zaidi zikifunga magoli 10 kati ya hayo 36, Chelsea ikishinda 4-0 wakiifunga Watford wakati Liverpool wao waliifurumusha Watford bao 6-1 na kukwea katika kilele cha ligi hiyo ikifikisha pointi 26 ikifatiwa na Chelsea yenye pointi 25.

● Katika mechi kali za wikiend hii ni ile ya London Derby ambapo Arsenal wakiwa nyumbani walishindwa kuifunga Tottenham Hotspur mchezo ukimalizika kwa sare ya bao 1-1 hali iliyoongeza wigo kwa Spurs ikifikisha mchezo wa 11 bila kufungwa.

● Manchester United baada ya kutoonja ushindi kwa mechi kadhaa jana walizinduka ugenini wakishinda bao 3-1 dhidi ya Swansea huku Zlatan Ibrahimovic akifunga mabao mawili na kuweka historia ya kufunga bao la 25,000 katika historia ya ligi kuu ya England huku Wayne Rooney akiwa mchezaji wa 3 katika historia ya ligi hiyo kutoa pasi iliyozaa goli kwa mara 100 baada ya Ryan Giggs na Frank Lampard.

● Sunderland nayo ilikua na wikiend njema sana kwa kupata ushindi wao wa kwanza msimu huu ikiifunga Bournemouth kwa bao 2-1 japokua ushindi huo umeshindwa kuwatoa katika nafasi ya mwisho.

● Ukiacha Arsenal ambao walihitaji ushindi ili kukalia kiti cha uongozi wa ligi hiyo lakini Manchester City nao wakaungana na Arsenal wakipata sare ya bao 1-1 dhidi ya Middlesbrough.

MATOKEO NA WAFUNGAJI WA MECHI ZOTE ZA WEEKEND HII

AFC Bournemouth 1-2 Sunderland

Dan Gosling (11')
                Victor Anichebe (33')
                Jermain Defoe (74') (Pen)

Burnley 3-2 Crystal Palace

Sam Vokes (2')
Johann Gudmundsson (14')
                  Connor Wickham (60')
                  Christian Benteke (81') (Pen)
Ashley Barnes (90'+3')

Manchester City 1-1 Middlesbrough

sbrough
Sergio Agüero (43')
                       Marten de Roon (90'+2')

West Ham United 1-1 Stoke City

Glenn Whelan (65') (Own Goal)
                         Bojan Krkic (75')

Chelsea 5-0 Everton

Eden Hazard (19' 56')
Marcos Alonso (20')
Diego Costa (42')
Pedro (65')

Arsenal 1-1 Tottenham Hotspur

Kevin Wimmer (42') (Own Goal)
                    Harry Kane (51') (Pen)

Hull City 2-1 Southampton

                   Charlie Austin (6') (Pen)
Robert Snodgrass (61')
Michael Dawson (63')

Liverpool 6-1 Watford

Sadio Mané (27' 60')
Philippe Coutinho (30')
Emre Can (43')
Roberto Firmino (57')
                    Daryl Janmaat (75')
Georginio Wijnaldum (90')

Swansea City 1-3 Manchester United

                    Paul Pogba (15')
                    Zlatan Ibrahimovic (21')
                    Zlatan Ibrahimovic (33')
Mike van der Hoorn (69')

Leicester City 1-2 West Bromwich Albion

                   James Morrison (52')
Islam Slimani (55')
                  Matthew Phillips (72')
************************************

Ligi itasimama mpaka jumamosi ya tarehe 19/11/2016 kupisha michezo ya kimataifa:
Na Ratiba ni hii baada ya mechi za kimataifa

3:30 PM - Manchester United vs Arsenal
6:00 PM - Crystal Palace vs Manchester City
6:00 PM - Everton vs Swansea City
6:00 PM - Southampton vs Liverpool
6:00 PM - Stoke City vs AFC Bournemouth
6:00 PM - Sunderland vs Hull City
6:00 PM - Watford vs Leicester City
8:30 PM - Tottenham Hotspur vs West Ham United

Jumapili 20/11/2016
7:00 PM - Middlesbrough vs Chelsea

Jumatatu 21/11/2016
11:00 PM - West Bromwich Albion vs Burnley

~Abel Alvaro

No comments

Powered by Blogger.