CHELSEA YANYANYASA NDANI NA NJE YA UWANJA MWEZI OKTOBA

Antonio Conte akiwa na tuzo yake 
Mwezi Oktoba ni mmoja kati ya miezi iliyokua ya furaha sana kwa mashabiki wa Chelsea baada ya kushinda michezo yake yote minne katika ligi kuu ya England mwezi huo.

Zawadi ya matokeo mazuri uwanjani ni pamoja na nje ya uwanja ambapo klabu hiyo imeweza kutwaa tuzo zote mbili za ligi hiyo katika mwezi wa Kumi ikitwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi na mchezaji bora wa mwezi.

Antonio Conte ambaye ni msimu wake wa kwanza akiwa na Chelsea ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwezi wa kumi akiwashinda Juggen Klopp wa Liverpool,Arsene Wenger wa Arsenal na Mark Hughes wa Stoke City.

Antonio Conte aliiongoza Chelsea kushinda mechi zote nne katika mwezi huo wa kumi huku ikimaliza bila kufungwa bao lolote.

Eden Hazard ndiye mchezaji bora wa mwezi wa kumi akiwa amechangia katika ushindi wa mechi zote nne akifunga magoli matatu dhidi ya Leicester City,Manchester United na Southampton.


No comments

Powered by Blogger.