BAADA YA KUICHEZEA SCOTLAND, ENGLAND NAO WAMWITA KARAMOKO DEMBELE TIMU YA TAIFA.
Jina la Karamoko Dembele limeendelea kushika vichwa vya habari duniani baada ya kipaji chake kukuna nyoyo za wadau wa soka wa Nchi Tatu ambazo Kijana huyu mwenye miaka 13 anaweza kuzichezea.
Karamoko Dembele mwenye kipaji cha hali ya juu katika kulisakata soka amesajiliwa hivi karibuni na Celtic katika kikosi cha vijana lakini wiki chache badae akaitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Scotland chini ya miaka 16 ambacho kilicheza dhidi ya Wales mwezi uliopita.
Hapo jana England nao wamemwita katika kikosi chao cha timu ya taifa chini ya miaka 16 ambacho kitacheza mwezi ujao dhidi ya Uturuki huku mwenyewe akionekana kufurahia na kupitia ukurasa wake wa Instagram alifurahia kuitwa huko.
Karamoko Dembele anaweza kuchagua kuiwakilisha nchi yoyote katika nchi Tatu ambazo ni Ivory Coast ambako wazazi wake ndiko walikozaliwa,England ndiko ambako yeye alikozaliwa miaka 13 iliyopita lakini pia Scotland ambako familia yake inaishi hivi sasa.
No comments