STOKE YAIBANIA MAN UNITED OLD TRAFFORD

Vibonde katika ligi kuu ya England msimu huu Stoke City wamekomaa na kuibuka na pointi moja katika pambano lao la ligi kuu ya England dhidi ya Manchester United.


Mchezo huo wa kwanza leo Jumapili katika ligi hiyo umeshuhudia kikosi cha Stoke City chini yaaMark Hughes ambacho hakijawahi kupata ushindi wowote msimu huu kikikomaa na kupata sare ya bao 1-1.

Manchester United itawabidi wajilaumu wenyewe baada ya kukosa nafasi nyingi za wazi huku kipa wa Stoke Grant akionekana ndiye shujaa wa mchezo huo baada ya kuokoa michomo mingi ya wazi.

Antony Martial aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Jesse Lingard alitangulia kufunga kabla ya Joe Allen hajaisawazishia Stoke City kufatia David De Gea kushindwa kudaka mpira ulioelekezwa langoni mwake.

Kwa matokeo hayo Stoke City wameongeza pointi moja na kufikisha pointi 3 baada ya michezo 7 huku United ikifikisha pointi 13.

No comments

Powered by Blogger.