SABABU HIZI NDIZO ZIMEFANYA MCHEZO KATI YA TAIFA STARS NA ETHIOPIA UFUTWE
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), limepokea barua kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Ethiopia
(EFF), ikielezea juu ya kufutwa kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliokuwa
ufanyike Oktoba 8, 2016.
EFF imesema kwamba imelazimika
kufuta mchezo huo ulikuwa kwenye kalenda ya FIFA kwa sababu za hali ya hewa si
rafiki kwa sasa nchini Ethiopia.
Kwa barua hiyo, Kocha Mkuu wa
Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface Mkwasa
atalazimika kuvunja kambi ya timu hiyo ambayo iliweka kwenye Hoteli ya Blue
Pear iliyoko Ubungo, Dar es Salaam.
Mchezo huo uliratibiwa kwa mujibu
wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo huwa na
kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa kwa wanachama wake – Tanzania ni miongoni
mwao. EFF, ndio walioomba nafasi hiyo.
Ingekuwa ni faida kwa Tanzania
kama ingeshinda mchezo huo kwa maana kina alama za nyongeza kama inatokea
unaifunga timu mwenyeji.
Matokeo yake yangekuwa ni sehemu
malumu kupima viwango vya ubora na uwezo wa timu za taifa. Kwa sasa Tanzania
inashika nafasi ya 132 kati ya nchi 205 wanachama wa FIFA zilizopimwa ubora.
Ethiopia yenyewe inashika nafasi ya 126.
Argentina inaongoza ikifuatiwa na
Ubelgiji anakocheza Mbwana Samatta – nyota wa kimataifa wa Tanzania. Samatta
anacheza klabu ya K.R.C Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji. Timu nyingine
bora kimataifa ni Ujerumani, Colombia na Brazil.
Katika Bara la Afrika, Ivory
Coast ambayo ni ya 34 kwa ubora duniani ndiyo inayoongoza ikifuatiwa na
Algeria, Senegal, Tunisia na Ghana.
No comments