PLUIJM ANAREJEA KWENYE BENCHI LEO, HIKI HAPA KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA MBAO

Baada ya wiki ndefu kwa kocha wa Yanga Hans Van Pluijm, akijiuzulu na kisha kurejea kwenye kikosi cha Yanga, jioni ya leo atakua na kibarua cha kutafuta pointi tatu mbele ya wabishi wa Mbao FC kutoka jijini Mwanza.


Pluijm amefanya mabadiliko katika kikosi chake leo akimrejesha beki Andrew Vicent kuchukua nafasi ya Calvin Yondani ambaye ataushuhudia mchezo huo akiwa jukwaani kutokana na maumivu ya mguu.

Thabani Kamusoko ataanzia benchi kumwachia nafasi Mbuyu Twite ambaye atashirikiana na Haruna Niyonzima katika eneo la kiungo.

Katika safu ya ushambuliaji, Amisi Tambwe ambaye amezidi kuongeza kasi ya ufungaji ataanza na Obrey Chirwa huku Donald Ngoma akisubiri katika bench.

Yanga wako nafasi ya pili katika msimamo wakiwa na point 24 pointi 8 nyuma ya Simba wanaoongoza

No comments

Powered by Blogger.