NDUGU, RIGOBERT SONG ANAHITAJI MAOMBI YAKO ILI APONE
Nahodha wa zamani wa Cameroon na beki wa Liverpool Rigobert Song anapigania maisha yake Hospitali baada ya kupata Stroke (Kiharusi).
Habari zinasema mchezaji huyo wa zamani mwenye miaka 40 amelazwa katika moja ya hospitali nchini Cameroon akipigania maisha yake.
Song ni mmoja ya wachezaji waliowika akiwa na Cameroon na Liverpool enzi za kocha Gerard Houllier na tayari wachezaji waliocheza naye kipindi hicho akiwemo Samuel Eto'o, Jamie Carragher na Robbie Fowler wametumia akaunti zao katika mtandao wa Twitter kumtakia apone haraka.
Song ambaye ni mjomba wa mchezaji wa zamani wa Arsenal na Barcelona Alex Song aliichezea Cameroon kwa miaka 16 akiitwa kwa mara ya kwanza katika fainali za kombe la dunia mwaka 1994 kule Marekani na mara ya mwisho mwaka 2010 katika fainali za kombe la dunia nchini Afrika Kusini.

No comments