MAPENZI YETU KWA SIMBA NA YANGA YAMEUZIDI HATA MPIRA WENYEWE.
Na Richard Leonce
Huwezi kupinga kwamba wapenzi wa soka hapa nchini wamegawanyika katika makundi mawili ya ushabiki wa timu kongwe za Simba na Yanga. Wapo wachache ambao hujipambanua kama wapenzi wa vilabu vingine kama vile Azam FC, Mtibwa Sugar, Coastal Union, Mbeya City nk. Lakini ukweli wao upo moyoni, ni lazima wanalalia upande mmoja kati ya Jangwani na Msimbazi.
Vilabu hivi vinapendwa kupita kiasi. Wajuzi wa mambo husema mapenzi yanapokuwepo ndipo hupatikana mahaba nami ni shuhuda wa mahaba mazito ya watanzania kwa vilabu hivi vikongwe.
Siyo kitu cha mara kwa mara kusikia mtu ametoa gari hata la kubebea mizigo tu kwa shule ya msingi aliyosoma, lakini ni kawaida sana kusikia tajiri ametoa gari la kutembelea kwa mchezaji mmoja anaemhusudu katika moja kati ya vilabu hivi.
Siyo vibaya kuipenda timu yako kwa kiasi hiki, lakini hofu yangu huja pale mahaba yetu kwa vilabu hivi yanapokua makubwa hadi kuuzidi mpira wenyewe. Pengine hii ni athari ya kihistoria. Historia inaonesha watu wengi walianza kuvipenda kwanza vilabu hivi kabla hata hawajafika uwanjani kuviona.
Soka kwenye vichwa vya wengi ilianza kupandikizwa na maneno yenye urembo wa watangazaji wa redio kama akina Ahmed Jongo na Dastan Tido Mhado ambao kwa bahati mbaya hata wao pia walikua na mahaba kwa timu zao za moyoni.
Kwa hiyo ni ukweli usiopingika kwamba Simba na Yanga zinapendwa kuliko unavyopendwa mpira wa miguu. Hii unaidhihirisha unapoona jinsi waamuzi wanavyoweweseka wanapochezesha mchezo unaozikutanisha timu hizi. Wengi husema rupia hupenyezwa lakini hata waamuzi nao madhali ni watanzania, ni lazima wanazo timu zao za moyoni.
Waswahili husema mapenzi ni upofu. Kuna kitu sasa hivi mitandaoni kinaitwa 'list of shame', ni orodha ya watu mashuhuri, wadau na wasio wadau wa soka ambao walikua wakichangishana fedha za kuwahamasisha wachezaji wa moja kati ya timu hizi kumfunga mpinzani wake kwenye mchezo uliowakutanisha Oktoba 1.
Inaitwa orodha ya aibu kutokana na aina ya majina yaliyomo kwenye orodha yenyewe. Jina moja lililonishangaza ni la aliyekua kocha wa timu inayoshiriki ligi hii hii nalo kuonekana kwamba limetoa mchango wa fedha ili timu yake ya moyoni ishinde. Timu ambayo ni tofauti na anayoifundisha. Unawaza kama huyu kocha anaweza kutoa fedha ili timu anayoshindana nayo kwenye ligi ishinde, itakuwaje siku timu anayoifundisha itakapokutana na hiyo timu yake ile ya moyoni?
Mapenzi yanakua upofu ambao hata wale wadau wa soka waliojaaliwa uelewa wa mambo hawawezi kuuzuia. Kila mwenye mapenzi na Simba anakuambia goli la Amisi Tambwe halikua goli halali na mwamuzi aliwabeba Yanga, Upande wa pili nao unadai goli alilofunga Ibrahim Ajib (lililokataliwa) lisingefungwa kama mwamuzi wa pembeni asingenyoosha kibendera kwa sababu kibendera chake kiliwafanya mabeki wao waache kumkimbiza mfungaji.
Ni wachache wanaoongea kwa uhalisia kwa maslahi ya mpira wa nchi na kuwasaidia wasio na uelewa wa kutosha, na hii ni kutokana na mahaba mazito kwa vilabu hivi viwili. Ataongea nini yule mchambuzi wakati hata yeye jina lake limo kwenye list of shame?
Vitu vingi vilivyooza hupakwa manukato ili vinukie ilimradi tu vinavi gusa vilabu hivi viwili. Mapema msimu huu uliibuka mjadala wa haki ya Azam FC kuutumia uwanja wao wa Azam Complex kwa mechi zote za nyumbani. Ni wazi kabisa hii ni haki yao na hakuna sababu zozote za msingi za kuwazuia Simba na Yanga kucheza Azam Complex wanapokua ugenini kwa Azam.
Lakini ni nani aliwatetea Azam? Hata mabosi wao wenyewe hawakuweza kwa sababu hata wao wana timu zao mioyoni kati ya hizi mbili. Hakuna chombo cha habari chochote kilichosimama kuitetea Azam FC katika kuidai haki yao hiyo. Badala yake wanahabari wakajikita kueleza jinsi usalama utakavyokua mdogo kwenye uwanja huo, na mapato kupungua ambayo kimsingi haikua hoja ya Azam.
Mtu anaipenda Simba kiasi cha kuamua kung'oa kiti cha uwanja wa taifa lake kuonesha hasira zake kwa mwamuzi. Hajali kwamba huo uwanja upo kwa ajili ya soka la leo, kesho na keshokutwa.
Kuna chombo cha habari za michezo ambacho huwa nakiandikia, wahariri wake walikataa kuchapisha habari niliyowapatia ingawa ilikua ni ya kweli lakini ilikua ni mbaya na ya aibu kwa moja kati ya vilabu hivi. Wakaniambia kabisa kwamba kuiandika hii ni kujitafutia matatizo, lakini chimbuko la yote ni mahaba yao ya dhati kwa klabu hiyo na kutokua tayari kuonesha uozo unaoihusu.
Ni lazima tutoke hapa, imefika mahali hata timu za taifa hatuzipendi kama tunavyozipenda hizi timu. Tunafika hatua tunawazomea wachezaji wa timu yetu ya taifa kwa sababu wanachezea vilabu ambavyo hatuvipendi. Hii inatokana na kuanza kuijua Simba au Yanga kabla ya Taifa Stars
Tunatia aibu kwa kweli na sijui ni nani atatuokoa kutoka kwenye penzi hili zito la mateso. Ajabu ni kwamba penzi lenyewe halivisaidii vilabu hivi kukua na kuongeza utajiri. Linavisaidia kupendeza tu kwa nje wakati ndani vinanuka ufukara uliokithiri

No comments