HATIMAYE UWANJA UTAKAOTUMIWA NA YANGA WAWEKA HADHARANI.

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea keshokutwa Jumatano Oktoba 12, 2016 kwa michezo saba huku ule mchezo kati ya Young Africans ya Dar es Salaam dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro ukipangwa kufanyika Uwanja wa Uhuru jijini.


Wakitumia Kanuni ya 6 kipendelea cha kwanza, Yanga wameutambulisha Uwanja wa Uhuru kama uwanja wa nyumbani kwa sasa baada ya kupeleka maombi Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF) ambako baada ya tathimini kwa mujibu kanuni hiyo ya sita, kipendelea cha sita, TFF imeiridhia.

Hatua hiyo inafuatia na Serikali ambao ni mmiliki wa viwanja vya Uhuru na Uwanja Mkuu wa Taifa, kuzuia vilabu vya Yanga na Simba kutumia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa michezo yao ya nyumbani kutokana na uharibifu.

No comments

Powered by Blogger.