KICHUYA AFUNGA 'GOLI LA MWAKA' KUSAWAZISHA 'GOLI LA MKONO' LA TAMBWE
Mpambano wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya Watani wa jadi wa jadi Yanga na Simba limemalizika kwa sare ya bao 1-1 huku kikubwa kinachozungumzwa ni goli la kusawazisha la Simba.
Shiza Kichuya alifunga goli hilo dakika ya 87 ya mchezo kwa njia ya mpira wa kona iliyoingia mojakwa moja katika goli la Yanga na kumwacha Kipa Ally Mustapha "Barthez" asijue la kufanya.
Tayari mashabiki walishaamini kwamba Yanga wataibuka na ushindi katika pambano hilo kufatia Simba kucheza wakiwa pungufu tangu kipindi cha kwanza kufatia kutolewa kwa kadi nyekundu nahodha Jonas Mkude lakini ilikuwa ndivyo sivyo kwani Simba licha ya kuwa pungufu walionekana kuwa makini muda wote.
Pambano hilo lilisimama kwa takribani dakika 10 baada ya Yanga kufunga goli huku mfungaji Amiss Tambwe akiwa ameshika mpira huo na mwamuzi kuruhusu liwe goli hali iliyoleta tafrani kwa mashabiki wa Simba na kupelekea mabomu ya machozi kupigwa kutuliza ghasia hizo.
Kwa matokeo hayo Simba wanaendelea kuongoza msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 17 wakifatiwa na Stand United wenye pointi 12 huku Yanga wakishika nafasi ya tatu na pointi zao 11.

No comments