HIZI HAPA AGENDA ZA MKUTANO MKUU WA YANGA JUMAPILI IJAYO

AJENDA ZA MKUTANO MKUU WA DHARURA WA WANACHAMA TAREHE 23 OKTOBA, 2016 KWENYE UWANJA WA KAUNDA.



1. SALA NA UTAMBULISHO WA WAGENI WAALIKWA:
1.1. Sala ya Wakristo ya Kubariki Kikao.
1.2. Sala ya Waislamu ya Kubariki Kikao.
1.3. Utambulisho wa wageni waalikwa waliohudhuria, pia wenye udhuru – Waziri wa Michezo na Sanaa; Mwenyekiti wa Baraza la Michezo (BMT), Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu Dar-Es-Salaam (DRFA) na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

2. KUFUNGUA KIKAO.

3. KUPITIA DONDOO ZA KIKAO KILICHOPITA CHA MKUTANO WA WANACHAMA NA KUIDHINISHA.

4. KUTHIBITISHA WAJUMBE WA BODI YA WADHAMINI NA KUMPUMZISHA MJUMBE MMOJA NA KUONGEZAMJUMBE MWINGINEKWENYE BARAZA LA WADHAMINI. MWENYEKITI KUOMBA RIDHAA YA KUMTEUA MJUMBE MMOJA BILA YA KUITISHA MKUTANO MKUU KUPUNGUZA GHARAMA KWAKLABU.

5. KUPITIA NA KUJADILL MUHTASARI YA MAKUBALIANO YA BODI YA WADHAMINI KULINGANA NA MAAGIZO YA WANACHAMAKUKODISHA TIMU YA YANGA NA NEMBO YA YANGA KWA KIPINDI CHA MIAKA KUMI/ NA KUPATA MAAMUZI KUPITIA KURA ZA WANACHAMA.

6. KUJADILI MWEYEKITI ABAKI KAMA MWENYEKITI AU KULINGANA NA MASLAHI YAKE KWENYE KAMPUNI, KAMA ITALETA MGONGANO KATIKAMPUNI YAKE INAYOKODISHA TIMU YA YANGA NA NEMBO YA YANGA KWA KIPINDI CHA MIAKA KUMI ILI KUPATA MAAMUZI KUPITIA KURA ZA WANACHAMA.

7. KURUDIA KUPITIA MAREKEBISHO YA KATIBA ILIYOAGIZWA NA WANACHAMA KUPITIA VIKAO VYAO MBALIMBALI NA BAADHI KUKATALIWA NATFF, BAADHI HAZIJASAJILIWA KAZI NA BMT NA BAADHI RITA WAMEZIKALIA BILA KUZIFANYIA KAZI KWA SABABU ZISIZOJULIKANA. KUPATA MSIMAMO WA WANACHAMA KWA KUZINGATIA KATIBA YA YANGA INAYOSEMA MIKUTANO YA WANACHAMA NDIO YENYE MAMLAKA YA MWISHO ILIMRADI TU MAAMUZI HAYO YAANGUKIE NDANI YA SHERIA ZA NCHI. NA SI SAHIHI VYOMBO HIVYO KUINGILIAA MAAMUZI HALALI YA WANACHAMA.

8. KUPITIA UTENDAJI WA KAMATI YA MASHINDANO, RATIBA YA LIGI KUU BARA, ADHABU YA YANGA KUTOKA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO AMBAYO ILISABABISHWA NA FUJO ZA MASHABIKI WA SIMBA.

9. KUPATA MAAMUZI JUU YA WANACHAMA AMBAO HAWAFIKI KATIKA MIKUTANO BADALA YAKE WANAKUWA WASEMAJI WA YANGA BILA KUWA NA MAMLAKA HAYO NA KULETA UCHONGANISHI WA WAZI NDANI YA KLABU, KUPOTSOHA JAMII NAKUCHAFUA MAJINA YA VIONGOZI WA KLABU.

10. TAREHE YA UCHAGUZI MDOGO KUJAZIA NAFASI ZILIZO WAZI NA KUPATA MWONGOZOWAKUTUMIA KATIBA IPI KATI YA 2010 AU 2014.PAMOJANA MASAHIHISHO BAADA YA 2014, AU BILA YA MASAHIHISHO YA 2014 YALIYOAMULIWA NA WANACHAMA.

11. HOTUBA YA MWENYEKITI –MAONI NA MSIMAMO WAKE JUU YA MAAZIMIO YA WANACHAMAKWENYE KIKAO; KUSEMA ANAYOYAJUA YA SIRI KUHUSU YANGA NA ADUI WA YANGA NA KUFAFANUA WANAOLETA VURUGU YANGA, BAADHI NI MAMLUKI WA WAFANYABIASHARA WENZAKE WALIOSHINDWA KUMSHINDA KWA NJIA HALALI NA SASA WANAITUMIA YANGA KAMA SEHEMU PEKEE ILIYOBAKI KUMUUMIZA KUPITIA MBINU ZINAZOTUMIKA HASA KWA KULETA VURUGU NDANI YA YANGA ILI KUMCHAFUA YEYE BINAFSI, KUFANYA KWAO HIVYO NI KUSHUSHA HADHI YA KLABU NA MAONI YAKE KWA MASLAHI YA YANGA, KIPI KIFANYIKE.

12. MENGINEYO.
13. SALA.
13.1. Sala ya Waislamu ya Kubariki Maamuzi ya Mkutano.
13.2. Sala ya Wakristo Kubariki Maamuzi ya Mkutano.

14. KUFUNGA MKUTANO.

No comments

Powered by Blogger.