AZAM NA YANGA HAKUNA MBABE, SIMBA WACHEKA KWA DHARAUUU

Pambano la ligi kuu ya soka Tanzania bara kati ya Mabingwa watetezi Yanga na Azam FC limemalizika kwa sare ya bila kufungana.


Pambano hilo lililomalizika muda mfupi uliopita katika dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam lilitawaliwa na ufundi mwingi katikati ya uwanja uliokosa maarifa ya kupata bao

Matokeo hayo ya Sare yanawapa Simba ambao ni vinara nafasi ya kutamba kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwani yanaendelea kuzidisha wigo wa pointi baina yao na Azam na Yanga.

Simba wapo kileleni wakiwa na pointi 23 wakati Yanga wakiwa na pointi 15 katika nafasi ya 3 Huku Azam wao wakijikokota katika nafasi ya 6 na pointi 12.

No comments

Powered by Blogger.