DAAAH HII KALI: GARI YA WAGONJWA YAMUOKOA VALENCIA ASIKAMATWE NA POLISI

Kwa wapenzi wa ligi kuu ya Uingereza, jina la Enner Valencia si geni kwao. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ecuador, anamilikiwa na West Ham United na yuko Everton kwa mkopo wa msimu mzima. Usiku wa kuamkia leo, Enner Valencia, 26, ametoa mpya baada ya kufanikiwa kuwakwepa polisi waliokuwa wakimsubiri kumkamata uwanjani alipokuwa anaichezea timu yake ya Ecuador dhidi ya Chile, kwa kutolewa na gari la wagonjwa nje ya uwanja.




KISA NI NINI HASA?
Inadaiwa kwamba, wanasheria wamewataka polisi kumkamata Enner Valencia kwa kushindwa kulipa pesa ya kumhudumia mtoto wake wa kike (hajatajwa jina), kiasi cha paundi 13,000 (takribani milioni 36.4 wza Kitanzania), pesa ambayo kisheria huko kwao Ecuador, baba hutakiwa kumhudumia mwanaye.

Mkasa huo ulitokea tarehe 06/10/2016, wakati wa mchezo wa kufuzu kombe la dunia 2018, kati ya Ecuador dhidi ya mabingwa wa Copa America-Chile, kwenye uwanja wa mjini Atahualpa mjini Quito, Ecuador, ambapo mwanzoni polisi walishindwa kumkamata Valencia wakati Ecuador wakifanya mazoezi ya kabla ya mechi, lakini wakaendelea kuwepo uwanjani hapo kumsubiri. Valencia alifanikiwa kuanza na kucheza mechi hiyo (akitengeneza pasi ya goli la kwanza la mechi hiyo waliyoshinda 3-0), na ndipo dakika ya 82 ya mchezo, inadaiwa kuwa alijifanya kaumia na kutolewa uwanjani kwa kitoroli maalum cha wagonjwa na kupelekwa kwenye gari la wagonjwa pembeni ya uwanja. Kabla hajapakiwa humo wakati huohuo polisi waliendelea kulifuatilia tukio hilo na kumkimbiza toka akiwa kabebwa kwenye kitoroli, na mpaka anapakiwa kwenye gari la wagonjwa bado polisi walilizingira ili wamkamate!
Inaaminika kuwa alipelekwa hospitali baada ya kutolewa uwanjani hapo.

Tukio hilo lilizua mshangao kwa mashabiki uwanjani hapo kwani si la kawaida kutokea. Wawakilishi wake wameahidi kulifuatilia na kulimaliza suala hilo. Inakadiriwa kuwa Enner Valencia analipwa takribani paundi 34,000 kwa wiki.

1 comment:

Powered by Blogger.