DIAMOND NA MBWANA SAMATTA WAMEVUNJA UKUTA.

Na Mandala J.
Ukiangalia kwa undani hapa muziki biashara sioni mwanamuziki wa kumfananisha na Diamond ni kama vile wachezaji wa Mpira waliopo sasa sioni wa kumfananisha na Edibily Jonas Lunyamila Mzee wa Mkasa wa Ujerumani, Mohammed Hussein Mmachinga ambae alikuwa anamkalisha kwenye mbao Nonda Shabani Papii sioni kama Madaraka Selemani au Zamoyoni Mogella hata Mbwana Samatta kiuwezo wa kufunga naamini hamfikii Zamoyoni Mogella DHL lakini uwezo wao Leo ndio majuto yao.



Kufanikiwa kwa Diamond ni Kazi nzuri ilioanza kufanywa na nyimbo ya CHEMSHA BONGO ya Prof Jay na ndio nyimbo ya chanzo cha mabadiliko katika nchi yetu kutokana na mashairi yake yaliofanya hata wale wazee walioona muziki ni uhuni walirudi kutega sikio na kutaka kujua kulikoni. Ikaja kuchagizwa zaidi na mashairi ya nyimbo za MAJI YA SHINGO, KAMANDA za Daz Nundaz , Upande wa pili wa Mpira uliendelea kuchukuliwa kama sanaa ya kujifurahisha baada ya Kazi na kuchukuliwa kama mchezo wa mapenzi kitu ambacho Leo hii ni hadithi kabisaa.

Nenda kamulize Juma Nature , Inspector Harun wanalia wanahuzunika lakini wamesahau kuwa wao ndio chanzo cha mafanikio haya ilibidi wengine waumie kwa manufaa ya wengine na kiukweli walifanya Kazi kubwa sana na hii ndio dhana ya maana halisi ya NENO UKOMBOZI.

Diamond,  hawa wanakosea wapi? Walikosea wapi? Wanatakiwa kufanya nini? Wewe ndie unaejua siri ya mafanikio ya muziki wa Bongo Fleva mpaka sasa ila maswali yangu huwezi kuyapa majibu ya kweli kabisaa kwa sasa maana ili mtu uendelee kufanikiwa endelea kuficha chanzo cha mafanikio yako ila tupe elimu ya nyavu juu ya kuvua samaki. Samaki maana tunahitaji nyavu zaidi ya Samaki.

Uwezo wa wanamuziki wa zamani ulisemekana na ulionekana ila tatizo  ni pamoja na Elimu , je? Diamond ana elimu gani? Hati miliki kama sababu je? Diamond ana ya kwake pekee yake? Wasambazaji je? Diamond anasambaza na kampuni nje ya sayari hii, kwa mafanikio ya Diamond kimuziki yanafuta vikwazo vyote vya maswali ya kufikirika na kujiaminisha kama sababu za kutofanikiwa kwa muziki na wanamuziki wetu. Kikubwa zaidi kimafanikio  kinabakia kuwa ni NIDHAMU kwa maana halisi ya maneno yanayounda hili neno maana ukiangalia wimbo wa MBAGALA uliushinda wimbo wa MGAMBO wa Juma Nature au kwakuwa ulikuwa wa mapenzi? Kikubwa utambuzi wa hitaji la soko na ushirikiano wa wadau wa muziki imekuwa ngao imara ya ushindi wa Diamond katika soko la muziki Tanzania na nchi za nje pia.

Diamond una kitu cha kutufundisha kama zawadi ya  nyavu kama Taifa  ili tukavue samaki bila ya kutupa siri ya chanzo cha mafanikio yake na kwa Mbwana Samatta hivyo hivyo maana kuna UKUTA umejengwa mkubwa katika uwezo na mafanikio ambao nyie mliuwekea ufa na sasa mmeubomoa na kufika yaliko mafanikio. Katika Mpira hadithi ya Edibily Jonas Lunyamila na kombe la Hedex pale Mwanza imeendelea kuwa  kama alama ya kutojua ya Kesho kama ilivyo kwa Haruna Moshi Boban na Jana nimesikia kwa Mrisho Ngassa na sio Ulimwengu pale DRC CONGO kwa upande huu wa Mpira  hakuna tatizo kubwa kufikia mafanikio ya Mpira zaidi ya uvumilivu na nidhamu ya kanuni za Mpira na kuachana na tamaa za pesa ndogo ndogo za viji zawadi vya mashabiki.
Hapa Tanzania mashabiki ndio chanzo kikubwa cha Mpira mbovu na matokeo mabovu na kutokuendelea kwa Mpira wetu.

Diamond watu walivuja jasho ulipo walipatamani wameshindwa hata ukimuliza wabunge ( Prof Jay) na SUGU watakuambia maana uwezo wanao lakini UKUTA uliopo kati ya uwezo na mafanikio ni mgumu kwao kimuziki na wameshindwa kuubomoa ikiwezekana toa msaada kwa jamii yote maana UKUTA uliopo katika UWEZO NA MAFANIKIO ni mgumu sana si sawa kati ya ule wa Elimu na Kazi.

Hawa wote niliowakumbuka na kuwa sema wanatamani kufikia ulipo japo muda au wakati kuwatupa mkono na kiburi cha muonekano wa mafanikio wanaweza kukataa ila wape msaada na waungwana hukubali kujifunza kama hawataki wache waisome namba.

Pamoja na kuwepo na matatizo yaliopo Diamond ameonesha njia ya kupita kufanikiwa na kuachana na kutegemea serikali kutatua matatizo hayo.

DIAMOND MSALIMIE NEYO.

0717-713403.


No comments

Powered by Blogger.