BAADA YA KUONDOKA PLUIJM, MKWASA AKATAA KUWA KOCHA MSAIDIZI YANGA

Siku chache baada ya aliyekua kocha wa Yanga Hans Van der Pluijm kutangaza kujiuzulu kuifundisha timu hiyo tetesi mtaani zimekua zikimuhusisha kocha wa taifa Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa kuwa kocha msaidizi wa Yanga.


Mkwasa amenukuliwa akikanusha habari hizo na kusema hajui zinakotokea na haoni mantiki ya yeye kuacha kazi akiwa kama kocha mkuu wa timu ya taifa na kwenda kuwa kocha msaidizi.

"Sijui wapi zinatoka habari hizi lakini sioni kama zina tija eti niache kazi yangu hapa nikawe kocha msaidizi" Alisema Mkwasa.

Licha ya Mkwasa kukanusha habari hizo bado wadau wa Soka la Tanzania wanaona upo uwezekano wa kocha huyo kwenda Yanga baada ya kuonekana hafurahishwi na baadhi ya mambo katika kikosi cha Taifa Stars.


No comments

Powered by Blogger.