YANGA YAREKEBISHA MAKOSA,AZAM YAACHA KILIO MBEYA,JULIO MAMBO MAGUMU
Ligi kuu ya soka Tanzania bara imeendelea leo katika viwanja vitano nchini na kushuhudia jumla ya magoli 11 yakifungwa.
Jijini Dar Es Salaam mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga baada ya kutoka sare katikati ya wiki huko Mtwara walirekebisha makosa yao na kuibuka na ushindi mnono wa bao 3-0 wakiwafunga Wana Lizombe Maji maji ya Songea.
Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Uhuru ulikua wa kwanza kwa Yanga kutumia uwanja huo baada ya marekebisho makubwa yaliyofanyika.
Amiss Tambwe alifunga mabao mawili na moja likifungwa na Deus Kaseke.
Huko Jijini Mbeya Azam FC wamemaliza mechi zao mbili huko kwa kupata ushindi 100% wakiwafunga Mbeya City bao 2-1 katika mchezo mkali uliopigwa katika dimba la Sokoine Jijini Mbeya.
Huko Mwadui mambo bado hayajakaa sawa kwa kocha wa timu hiyo Julio baada ya leo kupigana na kuambulia pointi moja tu wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani.
Mwadui ilitoka sare ya bao 2-2 na Stand United katika mchezo wa leo ikiwa ni siku chache baada ya kufungwa bao 1-0 na Kagera Sugar.
Katika dimba la Mabatini pale Pwani Ruvu Shooting waliifunga JKT Ruvu bao 1-0 wakati Ndanda FC wakiwa nyumbani walilazimishwa sare ya bila kufungana na Kagera Sugar.

No comments