TFF YAHAMISHA UWANJA MCHEZO WA AZAM NA SIMBA LAKINI SIKU INABAKI ILE ILE
Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara (VPL) kati ya Azam FC na Simba ya Dar es Salaam, utafanyika
Jumamosi Septemba 17, 2016 kama ilivyopangwa awali.
Mchezo huo utafanyika Uwanja
wa Uhuru, Dar es Salaam badala ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa sababu za
kuipa nafasi timu ya taifa ya vijana ya mpira wa miguu ya Congo Brazzaville
ambayo itakuwa nchini kwa ajili ya mchezo wa ushindani dhidi ya wenyeji –
Serengeti Boys ambayo ni timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka
17.
Timu hizo zinakutana kwenye
mchezo wa kwanza wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa
vijana wenye umri huo. Mchezo huo utafanyika Septemba 18, 2016 kwenye Uwanja wa
Taifa Dar es Salaam hivyo kutokana na kanuni za mashindano, siku moja kabla
mgeni anapata nafasi ya kufanya mazoezi.
Serengeti Boys ambayo ilipiga
kambi Shelisheli kujiandaa na mchezo huo ambako imejipanga vyema kuiondoa Congo
Brazzaville katika michezo miwili inayotarajiwa kuwa na ushindani mkali
ukianzia huo wa Septemba 18, 2016 kabla ya kurudiana jijini Brazzaville hapo
Septemba 30 au Oktoba 1 au Oktoba 2, mwaka huu.
Mtendaji Mkuu wa (CEO) Azam FC,
Saad Kawemba kwa mujibu wa kanuni ya 6 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
kipengele cha 5 na 6, ameridhia mchezo huo kufanyika Uwanja wa Uhuru hapo
Septemba 17, 2016 na kufuta upotoshwaji unaofanyika kwenye mitandao ya
kijamiii.
Kawemba alizungumza hayo, mara
baada ya kupokea Ngao ya Hisani halisi mara baada ya tuzo hiyo kufika jijini
Dar es Salaam ikitokea China pamoja na vifaa vingine. Itakumbukwa kwamba awali
Agosti 17, 2016 mara baada ya kuishinda Young Africans kwa mikwaju ya penalti,
Azam walipewa Ngao ya mfano.
No comments